Gemini kwenye Gmail
Okoa muda ukidhibiti kikasha chako nyumbani au popote ulipo ukitumia Gemini. Weka Gemini kwenye mpango wako wa Google One ya Juu kwa matumizi binafsi au kwenye mpango wako wa Google Workspace kwa matumizi ya kazini.
Andika barua pepe bora zaidi kwa usaidizi wa AI
Gemini kwenye Gmail inaweza kukutungia rasimu au majibu mazuri ili uweze kuyabadilisha, kuyawekea mapendeleo na kuyatuma kwa haraka.
Tafuta kwenye kikasha chako kwa njia mpya kabisa
Gemini inaweza kujibu maswali changamano kutoka kwenye kikasha chako au faili zilizo kwenye Hifadhi ya Google ili kukusaidia kupata unachotafuta.
Angalia maelezo muhimu, kwa muhtasari
Endelea kufuatilia mazungumzo marefu ya barua pepe ukitumia kipengele cha kuandaa muhtasari kilichojumuishwa.
Barua pepe salama, ya faragha na inayokupa udhibiti.
Hatutumii maudhui yako ya Gmail kwa madhumuni
yoyote ya matangazo
Gmail hutumia usimbaji fiche ambao ni bora katika
sekta hii kwa barua pepe zote unazozipokea na
unazozituma. Kamwe hatutumii maudhui yako ya Gmail
kukuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo.
Gmail inalinda usalama wa zaidi ya watu bilioni moja kila siku
Gmail huzuia aslimia 99.9 ya taka, programu hasidi na viungo hatari visifike kwenye kikasha chako kamwe.
Ulinzi wa kisasa zaidi uliopo dhidi ya wizi wa data binafsi
Barua pepe inayotiliwa shaka, ambayo huenda ikawa salama inapofika, Gmail hukujulisha na hivyo kukupa udhibiti.
Udhibiti bora zaidi wa barua pepe unazozituma
Hali ya Siri hukuwezesha kuweka tarehe ya mwisho ya kupatikana kwa barua pepe na huwataka wapokeaji wathibitishe kupitia SMS. Unaweza pia kuondoa chaguo za kusambaza, kunakili, kupakua na kuchapisha barua pepe.
Fanikisha mengi zaidi ukitumia Gmail
Endelea kuwasiliana na upange mambo yako
Anzisha Gumzo, jiunge kwenye simu ya video kupitia Meet au ushirikiane kwenye Hati, yote hayo moja kwa moja kwenye Gmail.
Fanikisha mengi haraka zaidi
Andika barua pepe na ujumbe haraka zaidi kwa kutumia vipengele kama vile Utungaji Mahiri ili uongeze muda wa kufanya mambo unayoyapenda.
Usisahau kujibu
Vidokezo vya kirafiki hukusaidia kudhibiti kila kitu.
Gmail inafaa zaidi kwenye programu
Jieleze kwa kutumia emoji
Miitikio ya emoji ni njia ya haraka na bora ya kujibu barua pepe, inayopatikana tu kwenye programu ya Gmail.
Tafuta barua pepe zako kwa urahisi
Kiolesura cha simu kilichorahisishwa kinaonyesha barua pepe ya kumkaribisha Helen kwenye timu, upau mkubwa wa emoji unaonyesha urahisi wa kujibu kwa kutumia emoji.
Badilisha kati ya akaunti moja na nyingine
Barua pepe zako zote za watoa huduma tofauti kwenye programu moja.
Tumia vipengele bora vya Gmail kwenye kifaa chako
Hufanya kazi na zana nyingine
Gmail hufanya kazi vizuri sana na programu za eneo-kazi kama vile Microsoft Outlook, Apple Mail na Mozilla Thunderbird, ikijumuisha usawazishaji wa anwani na matukio.
Endelea kuongeza tija, hata ukiwa nje ya mtandao
Gmail nje ya mtandao hukuwezesha kusoma, kujibu, kufuta na kutafuta barua pepe zako za Gmail wakati hujaunganishwa kwenye intaneti.
Tumia Gmail kwenye kifaa chochote
Furahia urahisi na wepesi wa Gmail, popote ulipo.
Gmail sasa ni sehemu ya Google Workspace
Shirikiana haraka, kwenye kifaa chochote, wakati wowote, yote katika sehemu moja.
Google Workspace ni mkusanyiko wa zana za tija na ushirikiano zinazosaidia watu binafsi, timu na biashara kufuatilia kila kitu. Ni suluhisho linaloweza kubadilika na la kiubunifu kwa ajili ya business au matumizi binafsi linalojumuisha programu zote unazopenda kama vile Gmail, Kalenda, Hifadhi, Hati, Meet na zaidi.
Pata majibu unayoyahitaji
Je, unahitaji usaidizi?
Tafuta vidokezo na miongozo ya hatua kwa hatua kwa watumiaji wa mara ya kwanza na wale wenye uzoefu.
Gmail imekuwa na msingi thabiti wa usalama tangu mwanzo. Tunajitahidi kukulinda dhidi ya taka, wizi wa data binafsi na programu hasidi kabla hazijafika kwenye kikasha chako. Nyenzo zetu za kuchuja barua taka zilizoimarishwa kwa AI huzuia takribani barua taka milioni 10 kila dakika.
Hapana. Ingawa unaweza kuona matangazo kwenye akaunti yako ya Gmail unayoitumia bila malipo, barua pepe zako ni za faragha. Google haichanganui au kuchakata maudhui ya Gmail kwa madhumuni ya utangazaji.
Ingawa vipengele vya Gmail vina usalama wa kutosha kwa wengi wa watumiaji, baadhi ya akaunti zinaweza kuhitaji viwango vya ziada vya usalama. Mpango wa Ulinzi wa Kina wa Google unawalinda watumiaji maarufu na wenye maelezo nyeti ambao wamo katika hatari ya kulengwa na mashumbulio ya mtandaoni.
Pata maelezo zaidi
Gmail ni sehemu ya Google Workspace ambapo unaweza kuchagua mipango tofauti. Pamoja na kile unachokipenda kuhusu Gmail, unapata anwani maalum ya barua pepe (@yourcompany.com), idadi isiyo na kikomo ya anwani za barua pepe za kikundi, hakikisho la asilimia 99.9 la muda wa kutumika, nafasi ya hifadhi ambayo ni maradufu ile ya Gmail ya kibinafsi, bila matangazo, usaidizi wa saa 24 kwa siku 7 za wiki, Google Workspace Kusawazishwa na Microsoft Outlook na mengineyo.
Pata maelezo zaidi
Je, unahitaji usaidizi?
Tafuta vidokezo na miongozo ya hatua kwa hatua kwa watumiaji wa mara ya kwanza na wale wenye uzoefu.
Onyesha ulimwengu
umahiri wako.
umahiri wako.
Anza kutumia Gmail iliyo mahiri zaidi.